Shirikisho la soka duniani FIFA limemsimamisha kazi, katibu mkuu wake, Jerome Valcke kufuatia uchunguzi wa kifisadi unaoendelea kufanywa ndani ya shirikisho hilo.

Taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia hii leo imeeleza kwamba, kamati ya juu ya uongozi wa shirikisho hilo, imemsimamisha kazi Valke kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi ambao unaendelea kufanyika kufuatia ubadhilifu wa tiketi za fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kamtibu mkuu huyo alikiuka maadili ya kazi yake kwa kujiingiza kinyemela katika mtandao wa uuzaji wa teketi za fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 zilizofanyika nchini Brazil.

Hata hivyo uchunguzi huo unaendelea kuchukua nafasi yake huko mjini Zurich na kama itabainika Valke alijihusishwa kikamilifu na janga hilo, atafikishwa kwenye kamati ya maadili ya FIFA kujibu tuhuma zitakazomkabili.

Valke amekua kazini tangu mwaka 2007 na amekua na uhusiano wa karibu na rais wa FIFA Sepp Blatter na wakati mwingine alionekana kutetea uovu uliofichuliwa na maafisa wa upepelezi kutoka nchini Marekani FBI, tangu mwezi May mwaka huu ambapo baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo walitiwa nguvuni.

Luke Shaw Kupigwa Kisu Tena
Kauli Ya Bulembo Wa CCM Kuhusu Ikulu Yazua Utata