Meya wa halmashauri ya manispaa ya Ilala, mheshimiwa Jerry Slaa ametangaza nia ya kugombea kiti cha ubunge wa jimbo la Ukonga, hali inayoashiria kutokigusa tena kiti cha umeya wa halmashauri hiyo anachokikalia hivi sasa.

Slaa ametangaza uamuzi wake kupitia akaunti yake ya Instagram na kueleza kuwa leo (Julai 6) itakuwa siku ambayo halmashauri hiyo itafanya kikao chake cha mwisho cha Baraza la Madiwani.

Slaa ameandika:
Kesho ndio siku ya mwisho kwa Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Tunaahirisha vikao mpaka baada ya Uchaguzi. Kwa kuwa sigombei tena Udiwani sintaweza gombea umeya. Hii ndio sikuyangu ya mwisho kufanya kazi za umeya. Namshukuru sana Mungu nimemaliza salama. Naamini atayechaguliwa atafanya kazi kwa moyo wake wote kuwahudumia wananchi. Mungu akipenda nitakuwa mjumbe wa Baraza kwa kiti cha Ubunge wa Ukonga.

Slaa ataingia kwenye mchakato wa chama chake wa kumteua mgombea ubunge kupitia kura za maoni kabla ya kusimama kuwania kiti hicho katika uchaguzi mkuu, Oktoba mwaka huu.

Diamond Anatarajia Kubeba Tuzo Sita Kubwa Za Kimataifa
Diamond Ampa AY Shukurani Na Heshima Ya Pekee