Mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain wamesitisha mkataba wa mshambuliaji kutoka nchini Hispania Jesé Rodríguez Ruiz, ambao ulikua umesalia na miezi sita kabla ya kufika kikomo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alisajiliwa PSG mwaka 2016 akitokea kwa mabingwa wa soka nchini kwao Hispania Real Madrid mwaka 2016, lakinia lipelekwa kwa mkopo katika vilabu vinne tofauti.

Jese ametumika mara mbili kwenye kikosi cha PSG msimu huu akitokea benchi benchi kwenye michezo ya ligi ya Ufaransa (Ligue 1). lakini, baada ya kukabiliwa na changamoto kadhaa ya nje ya uwanja katika siku za karibuni, PSG wameamua kukatisha mkataba wake.

PSG wamethibitisha taarifa hizo kupitia tovuti yao rasmi jana Jumapili (Desemba 06): “Paris Saint-Germain inamtakia Jese kheri katika kipindi chote cha taaluma yake.”

Jese anaondoka mji mkuu wa Ufaransa (Paris), akiwa amefunga mabao mawili katika michezo 18 kwenye mashindano yote.

Miquissone awaachia kumbukumbu Plateau United
Mwinyi, Maalim Seif waungana