Jeshi la Azerbaijan limeeleza kuwa lilipoteza wanajeshi mashujaa 2,802 katika operesheni iliyofanyika Nagorno-Karabakh kukomboa wilaya zake kutoka kwa uvamizi.

Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan imetoa upya taarifa juu ya idadi ya waliopoteza maisha katika mapigano yaliyoanza mnamo Septemba 27 na kumalizika Novemba 10 baada ya makubaliano kutiwa saini kufuatia kukubali kushindwa kwa Armenia.

Katika taarifa iliyotolewa, imearifiwa kuwa idadi ya wanajeshi mashujaa waliofariki, ambayo hapo awali ilitangazwa kuwa 2,783, iliongezeka hadi kufikia 2,802 baada ya ugunduzi wa makaburi kadhaa na vitambulisho vyao.

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa zaidi ya wanajeshi mashujaa 60 waliouawa bado hawajatambuliwa, na kufahamisha kuendelezwa kwa juhudi za kuwatambua na kuwapata wanajeshi 40 walipotea.

Baada ya ukombozi wa vituo vya miji 5, wilaya 4 na vijiji 286 katika operesheni iliyozinduliwa na jeshi la Azerbajain mnamo Septemba 27, Armenia ilikubali kushindwa na kutia saini makubaliano ya kuahidi kuhamisha maeneo ya Aghdam, Lachin na Kelbajar.

Jeshi la Armenia liliondoka Aghdam Novemba 20, likatoka Kalbajar mnamo Novemba 25 na kutoka Lachin mnamo Desemba 1.

Nkamia achukua fomu Simba SC
Aweso: RUWASA kamilisheni miradi yenye changamoto