Katika kuhakikisha kuwa Jeshi la Magereza nchini linaunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli za kuibadilisha nchi kuwa Tanzania ya Viwanda, jeshi hilo limeanza kutekeleza mpango wake wa kufufua Kiwanda chake cha Sukari na Kilimo cha Miwa katika Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro kwa lengo la kuongeza kiwango cha upatikanaji wa Sukari nchini.

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa ambapo amesema kuwa kuwa katika kutekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda, Jeshi la Magereza limeainisha baadhi ya Miradi inayoweza kuiweka Tanzania katika Uchumi wa Viwanda ikiwemo ufufuaji wa Kiwanda hicho na Kilimo cha Miwa katika Gereza lake la Mbigiri Mkoani Morogoro.

Amesema kuwa kwa kwa kushirikiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii PPF na NSSF,  Jeshi hilo limeanza zoezi la kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha Miwa katika Gereza la Mbigiri mkoa wa Morogoro.

 

 

“Ni matumaini  yetu  hadi kufikia  mwisho wa mwaka huu kiwanda hiki kitaanza kufanya kazi ufufuaji wa kiwanda hiki utawaneemesha wakulima wadogo wadogo  wa miwa (Outgrowers) waliopo maeneo yanayolizunguka gereza la Mbigiri mkoa wa Morogoro na hivyo kuinua hali zao za kiuchumi kwa kuwa itakuwa ni fursa ya wakulima hao kupata soko la uhakika na karibu zaidi kwa ajili ya kuuza bidhaa zao baada ya kuvunwa kwenye mashamba yao’’. amesema Dkt. Malewa

Hata hivyo, Dkt. Malewa ameongeza kuwa pamoja na ardhi yenye rutuba ambayo kwa Jeshi la Magereza linaiona ni fursa ikitumiwa vizuri, lakini pia ipo Miundombinu mbalimbali inayoweza kusaidia kuanzisha Viwanda na ardhi hiyo inaweza kutumika katika shughuli za kilimo na hivyo kuongeza uzalishaji wa chakula hapa nchini.

Mchezo Wa Kirafiki Kati Ya Gor Mahia Na Everton
Mwakyembe avunja baraza la michezo Tanzania