Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa Wananchi (CNSP), chombo kilichoundwa na kundi la jeshi lililofanya mapinduzi nchini Mali, Agosti 18, imefanya uteuzi wa viongozi katika nyadhifa mbalimbali.

Cheick Oumar Traoré, ameteuliwa kuwa mshauri maalum wa kiongozi wa mapinduzi, anayehusika na habari na mawasiliano na daktari Youssouf  Coulibaly ambaye ni raia ameteuliwa, kuwa mshauri maalum wa kiongozi wa mapinduzi, anayehusika na maswala ya kisheria.

Kwa upande wa jeshi, Jenerali Souleymane Doucouré, kiongozi wa zamani wa msemaji wa sasa wa kundi la jeshi lililofanya mapinduzi ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya ulinzi, Jenerali Oumar Diarra, akiteuliwa kuwa mkuu mpya wa jeshi la Mali.

Wakati huohuo, aliyekuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita (IBK), amelazwa hospitalini tangu Jumanne wiki hii katika hospitali moja mjini Bamako, ingawa mmoja kati ya wasaidizi wake amesema kuwa Keita amekwenda kufanya vipimo vya kawaida vya afya yake hospitali.

Mwanasiasa huyo wa miaka 75 alizuiliwa kwa siku kumi na wanajeshi kabla ya kujiuzulu na baaadae kuachiliwa huru.

Simba SC, Young Africans patachimbika 2020/21
Membe: Tutakuwa mishumaa, haibiwi mtu, ni kivumbi