Jeshi la Myanmar leo Februari 1, 2021 limetwaa madaraka katika mapinduzi ambayo hayakuwa ya umwagaji damu, na kumshikilia kiongozi wake aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia Aung San Suu Kyi na kutangaza hali ya hatari ya mwaka mmoja.

Hatua hiyo imefikisha mwisho muongo mmoja wa utawala wa kiraia nchini Myanmar, huku jeshi likihalalisha mapinduzi yake kwa kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi wa Novemba ambao chama cha Suu Kyi cha National League for Democracy – NLD kilipata ushindi wa kishindo.

Jeshi kupitia kituo chake cha televisheni limetangaza kuwa Jenerali wa zamani Myint Swe atakuwa Kaimu Rais kwa mwaka mmoja.

Suu Kyi ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, na Rais Win Myint walikamatwa katika mji mkuu wa Naypyidaw kabla ya alfajiri, saa chache tu kabla ya Bunge kuanza vikao vyake kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi huo.

Majaliwa anena hili kwa makampuni binafsi
Kiswahili champandisha cheo Jaji