Jeshi la Polisi nchini Kenya limewataka Wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari kuhusu vitisho vya uwezekeno wa kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi kipindi Cha krismasi na Mwaka mpya.

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo Hillary Mutyambai amewataka Wananchi kuwa waangalifu katika maeneo ya kuabudu  na katika vituo vya usafiri wa umma.

Amesema hayo baada ya Jeshi la Polisi nchini humo kuwakamata washukiwa wa ugaidi wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi la Al-shabaab kutoka nchini Somalia baada ya kutekwa kwa wafanyakazi wanne wa kampuni ya ujenzi ya Kaskazini Mshariki mwa Nchi hiyo.

Lichaya juhudi kubwa zinazofanywa na lakini Jeshi la Polisi limesema  bado kuna tishio na Kila mwananchi anastahili kuwa makini wakati huu wakipindi cha sikuku za mwisho wa Mwaka na kwamba litaimarisha usalama katika maeneo yote.

Mchezaji Manchester United kutua Barcelona
Serikali yatoa msimamo UNHCR kuvunja makubaliano