Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuwasaka na kuwahoji watu wanaobeza juhudi zake pamoja na kushabikia matukio ya uhalifu mitandaoni.

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani jana aliwaambia waandishi wa habari baada ya kuwaonesha eneo la tukio la mauaji ya askari wanne wa jeshi hilo eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Marijani.

Tamko hilo la Marijani lilikuja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuagiza walioandika kufurahia mauaji hayo wakamatwe.

Kamishna Marijani alieleza kuwa katika tukio hilo, mwajambazi walipora bunduki mbili aina ya SMG na risasi 60 lakini hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki ya CRDB waliyokuwa wanalinda askari hao, jambo lilitoa picha kuwa walilenga kuwashambulia askari polisi.

Alisema tukio hilo ni sawa na kutangaza vita na Jeshi hilo hivyo watawasaka na kuwachukulia hatua stahiki.

Salama Jabir afunguka adhabu aliyopewa na Mwana FA baada ya 'kumponda'
Mbowe afunguka kuhusu kunyang’anywa Jengo la Club Bilicanas