Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi kutokuwa na hofu kutokana na picha zinazosambaa zikiwaonesha askari wake wakiwa kwenye mazoezi katika maeneo mbalimbali nchini.

Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)

Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa na msemaji wake, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Advera Bulimba zimeeleza kuwa askari hao wanafanya mazoezi ya kawaida na hayalengi kuzuia shughuli zozote zinazofanywa kihalali.

“Jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi,” amesema Bulimba.

Picha mbalimbali za askari wa jeshi hilo wakifanya mazoezi zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii huku ikiaminika kuwa wanajiandaa kuzuia maandamano na mikutano ya Chadema kupitia Operesheni waliyoipa jina la UKUTA.

Video: Huu Ukuta utabomoka tu, kwa Dar es salaam umeshabomoka - Simon Sirro
Hamisa Mobeto azungumzia uhusiano wake na Diamond