Jeshi la Polisi Nchini, limetembelea Hifadhi ya Taifa ikilenga kujionea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ambayo inapatikana ndani ya mkoa wa Arusha, sambamba na kuhamasisha watu kutembelea vivutio hivyo.

Akiongoza zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, CP Awadh Haji alisema wameona fahari kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali ikiwa ni kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais za kuutangaza utalii wa Nchi yetu.

Amesema, ziara hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha uhusiano, kutatua changamoto za kiusalama baina ya Jeshi hilo na wadau wengine wanaohusika moja kwa moja kuhudumia watalii ambapo waimeingia mkataba wa mashirikiano na Chuo cha Taifa cha Utalii, ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji Maafisa, Wakaguzi na Askari.

Amesema, ‘’dhamira ya Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu ni kukuza Utalii wa nchi yetu na kuongezeka idadi ya watalii nchini, hivyo sisi Jeshi la Polisi tutahakikisha tunaenda kutoa huduma bora kwa watalii na wageni wanaofika nchini sambamba na kuimarisha usalama wao.

Kwa upande wake, Mhifadhi wa Hifadhi hiyo ACC Yusta Kiwango alisema wamekua na mahusiano mazuri na jeshi la Polisi ambapo mara nyingi hufanya operesheni za pamoja hali ambayo inapelekea Watalii wanaotembelea hifadhi hiyo kufurahia mandhari bila ya uwepo wa changamoto za kiusalama.

Aidha ametoa wito kwa taasisi nyingine za serikali na za binafsi kutembelea hifadhi hiyo ili kujionea vivutio vilivyopo sambamba na kuutangaza utalii wa Nchi yetu na ziara hiyo imekuja mara baada ya Jeshi hilo kuingia mkatabata wa mashirikiano na Chuo cha Taifa cha Utalii jana Jijini Arusha ambapo maafisa wa Jeshi hilo watajengewa uwezo wa kiutendaji wa namna bora ya kuwahudumia watalii.

Hakuna wa kuichonganisha Msomera, Serikali - CCM
GGML yasaidia vifaa tiba kuboresha Sekta ya Afya