Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Safia Jongo, amesema kuwa jeshi hilo limekamata Bastola aina ya Trurus ambayo imetengenezwa nchini Marekani, ikiwa na risasi 5 pamoja na magazine yake na iliyokuwa inamilikiwa bila kibali halali.

Kamanda ACP Jongo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya mwezi Oktoba, 2021 ambapo ameeleza pia wamegundua kiwanda cha kutengenezea bunduki za kienyeji aina ya Gobore baada ya msako mkali kuendeshwa na Jeshi la Polisi.

Tulifanikiwa kumkamata mtu mmoja mwanaume ambaye alikuwa na mtambo wa kutengeneza hayo magobore na alikuwa na magobore 11, pamoja na vifaa vya kutengeneza silaha, kama Trigger, Cockinhandle ambayo inatumika katika silaha hizo”, alisema ACP Jongo.

“Operesheni ilipangwa kimkakati tumekuwa na matumizi mabaya ya silaha hizo aina ya gobore katika misitu yetu, hivyo ikatulazimu kupanga mikakati kujua ni wapi yanapotoka”ACP Jongo

Hata hivyo ameongeza kuwa kwenye operesheni hiyo wamekamata kilo 372 za mirungi pamoja na pikipiki 12 ambazo zilikua zikisafirisha mirungi na wahamiaji haramu.

Sakata la GSM lafikishwa Serikalini
Young Africans na mpango wa kumsajili Chama