Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi amethibitisha kwa jeshi hilo linamshikilia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa mahojiano.

Amesema kuwa kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia jana Jumatano Julai 21 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana alikokifikia.

“Baada ya kumkamata, wenzetu wa Dar es Salaam nao walitueleza kuwa wanamtafuta kwa makosa mengine anayodaiwa kuyafanya huko; hivyo tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam anakoendelea kuhojiwa,” amesema Kamanda Ng’anzi.

Amesema kuwa kiongozi huyo wa CHADEMA yupo kwenye mikono salama ya polisi Mkoa wa Dar es Salaam na atarejeshwa Mwanza baada ya mahojiano ili aunganishwe na wenzake 15 wanaoshikiliwa kuhusiana na kongamano la Katiba Mpya lililozuiwa na jeshi hilo jana.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia
Kilo 164 ya samaki wamekufa ufukwe wa Dar es Salaam