Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ambaye ni Amri jeshi Mkuu wa Jeshi la Sudan Kusini ameridhia kubadilishwa kwa jina la jeshi la nchi hiyo kutoka jeshi la ukombozi la watu wa Sudan (SPLA) na kuwa Jeshi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF).

Uamuzi huo ulifikiwa hivi karibuni baada ya kujadiliana na mabaraza ya kamati sita za jeshi hilo.

Mabadiliko hayo yanamaanisha kuwa kaunzia sasa litakuwa ni jeshi linaloendeshwa na wananchi wote wakiwemo waliokuwa upande wa waasi ili kuwatumikia raia wa Sudan Kusini.

SPLA ilianzishwa mwaka 1982 ikiwa kundi la waasi lililopambana katika vita ya pili vya wenyewe kwa wenyewe Sudan, kabla ya kujitenga kwa Sudan Kusini iliyopewa  hadhi ya nchi kamili mwaka 2011.

Kufikia mwaka 2013 SPLA ilikadiriwa kuwa na askari takribani 210,000.

 

Msigwa mbaroni, apigwa 'stop' mikutano ya hadhara
Abiria wa Ukerewe wagoma