Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ tayari ipo kambini kujiandaa na mechi ya Kundi F dhidi ya Niger kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika ‘Afcon 2023’ itakayopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku timu hiyo ikihitaji ushindi kwa lengo la kujiweka pazuri kwenda Ivory Coast.

Stars imeingia kambini kwa baadhi ya wachezaji waliojulishwa kambi hiyo, huku orodha kamili ya timu hiyo itatangazwa leo na Kocha Mkuu, Adel Amrouche.

Timu hiyo, inayoshika nafasi ya pili kwenye Kundi F lenye vinara Algeria iliyofuzu tayari kwenye fainali hizo za mwakani, Uganda iliyopo nafasi ya tatu na Niger inayoburuza mkia huo ni mchezao muhimu kutokana na ukweli ikishindwa kuvuna pointi tatu itajiweka pabaya.

Stars na Uganda kila moja ina pointi nne baada ya kucheza mechi nne, huku Niger ikiwa na mkiani huku ikiwa na rekodi mbaya kwa mechi za nyumbani kwenye kundi hilo baada ya awali kulala 2-0 kwa Algeria na kisha kufungwa 1-0 na Uganda kwenye mchezo uliopita.

Kama Stars itashinda itafikisha alama saba na kujiweka pazuri kuungana na Algeria ambayo wikiendi hii itavaana na Uganda kabla ya mechi za mwisho zitakazopigwa Septemba 4 kwa Stars kuifuata Algeria na Uganda kumalizana na Niger.

Ikumbukwe katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo, Stars na Niger zilitoka sare ya 1-1, na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo amesema wachezaji walioitwa tayari wapo kambini.

“Kikosi kimeingia kambini na wachezaji walioitwa wameripoti,” amesema Ndimbo

Wakati huo huo Kocha Mkuu wa Taifa Stars Adel Amrouche ametangaza kikosi cha timu hiyo ambacho kitaivaa Niger mwishoni mwa juma hili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

WALINDA LANGO: Metacha Mnata (Yanga), Beno Kakolanya (Simba), Vuai (KMKM) na Zuberi Foba (Azam)

MABEKI: Datus Peter (Kagera), Dickson Job, Kibwana Shomari, Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca (Yanga), Zimbwe Jr, Kennedy Juma (Simba), Novatus Dismac (Zulte, Ubelgiji), Abdi Banda (Chippa, South Africa) na Lameck Lawi (Costal)

VIUNGO: Himid Mao Mkami (Ghazl, Egypt), Adolph, Aziz Andambwile (Singida), Muzamir Yassin (Simba), Mudathir Yahya (Yanga), Ayoub Idrissa Bilal (Ankara, Uturuki), Ben Starkie (Basford Utd, England) na Morris Abraham (Spartak Subotica, Serbia)

WASHAMBULIAJI: Simon Msuva (Al Qadsiah, Saudi), Abdul Suleiman Sopu (Azam), Kibu Dennis (Simba), John Tiber, Bernard Kamungo (FC Dallas, USA), Adi Yusuph (Brackley Town, England) na Mbwana Samatta (Genk, Ubelgiji)

Kujiunga vyama vya wafanyakazi ni hiari - Serikali
Lionel Messi: Sidhani kama nitacheza 2026