Klabu ya Young Africans imetangaza kikosi cha wachezaji 19 kitakachoshiriki Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA KAGEME CUP’ itakayoanza jijini Dar es salaam mapema mwezi ujao.
Katika kikosi hicho Young Africans imewataja wachezaji Dickson Ambundo anayecheza nafasi ya kiungo na beki David Brayson, ambao inasemekana tayari wameshasajiliwa na klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Young Africans pia itawatumia wachezaji sita wazoefu wakiongozwa na nahodha msaidizi, kiungo Mukoko Tonombe ambaye amewaambia mabosi wake hatarudi nyumbani na badala yake atabaki kupambana.
Mbali na Mukoko, wengine ni Ramadhan Kabwili, Paul Godfrey ‘Boxer’, Dickson Job, Zawadi Mauya, na Waziri Shentembo.
Mastaa hao watachanganyika na vijana chini ya miaka 20 ambao ni kipa Geofrey Magaigwa, mabeki M Msenda, Said Mashoto, R Msonjo na Ally Said, viungo Omary Chibada, S Kwangala, J Guber, Best Kahemela na washambuliaji Abby Mikimba, A Yunus.
Katika michuano ya ‘CECAFA KAGAME CUP 2021’ Young Africans imepangwa kundi C na Express FC (Uganda) na Nyassa Big Bullets (Malawi).