Jengo moja lililopo katika mtaa wa India jirani na Sabodo Parking Tower jijini Dar es salaam limeshika moto mchana huu ambapo vikosi vya zimamoto vimefika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima.
Watanzania wenye asili ya kihindi wakiwa kwenye kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam, kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam,kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakijiandaa kupokea waathirika wa janga la moto katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi, jijini Dar es Salaam, kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Jengo la ghorofa 12 lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi lililoshika moto na kufanikiwa kuzimwa na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,leo jijini Dar es Salaam.
Kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuzima moto, kuokolea watu na mali kwenye majengo marefu, kikisaidia uokoaji katika jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi, jijini Dar es Salaam, baada ya kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.