Jeshi la zimamoto na uokoaji limewataka wananchi kuhakikisha wanachukua tahadhari zote za kudhibiti vyanzo vya moto mara baada ya kuanza kwa kampeni za vyama vya siasa.

Mkaguzi Michael Bachubira, ambaye ni Afisa operasheni mkoa wa kizimamoto Temeke, amesema mara nyingi uzoefu umeonyesha kuwa kipindi cha kampeni kumekuwepo na mihemuko hususan kwa wakereketwa.

Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa  kupeana zamu kwenda kwenye mikutano ya kampeni ili kuhakikisha nyumba inabaki na mtu mwenye uelewa wa kutoa taarifa endapo litatokea janga la moto.

Aidha, ameitaka jamii kuacha dhana kwamba mara baada ya wananchi kuripoti tukio, gari huwa linaondoka bila maji huku akielezea utayari wa jeshi hilo hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kuhakikisha jamii inakuwa salama.

Ruksa wanafunzi wajawazito kuendelea na masomo- Zimbabwe
Muigizaji wa ‘Black Panther’, Boseman afariki dunia