Jeshi la Zimbabwe limekanusha madai kuwa mapinduzi ya kijeshi yamefanyika kuiondoa serekali, na kudai kwamba rais Robert Mugabe na familia yake wapo salama.

Katika taarifa iliyotolewa na jeshi kupitia televisheni ya taifa, imesema kuwa jeshi linalenga wahalifu wanaosababisha shida za kijamii na kiuchumi na kuwafikisha mbele ya sheria ili waweze kushughulikiwa.

Aidha, magari ya jeshi na wanajeshi wamekuwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Harare baada ya wanajeshi hao kushikili shirika la serikali la utangazaji la nchi hiyo ZBC, hivyo kusababisha hofu kubwa kwa wananchi wa nchi hiyo.

Msemaji wa ubalozi wa Marekani mjini Harare, amesema kuwa mitaa ya Harare ni tulivu na hakuna magari yeyote ya jeshi vikiwemo vifaru ambavyo vimeonekana vikipiga doria mitaani.

Hata hivyo, hali ya wasiwasi ilizuka wiki iliyopita wakati rais Robert Mugabe alipomfukuza makamu wake, Emmerson Mnangagwa na kumshutumu kwa kutomtii na kupanga kutwaa madaraka.

Majaliwa aitaka wizara kufanya utafiti wa kina
Masha awaweka njiapanda Chadema