Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, limethibitisha kuwa Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mzee Philip Mangula aliwekewa sumu na uchunguzi wa aliye husika bado unaendelea.

Imeelezwa kuwa Mangula alidondoka ghafla mnamo Februari 28, 2020 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM iliyokuwa ikijadiri mambo mbalimbali ya chama likiwemo suala la adhabu ya wanachama watatu.

Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa leo Machi 9, 2020, walianza uchunguzi wa tukio hilo baada kupokea taarifa kutoka kwa uongozi wa CCM.

“ Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, lilishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na taasisi mbalimbali limebaini kwamba ndani ya mwili wa mzee Mangula kulikuwa na sumu. Uchunguzi kuhusu namna sumu hiyo ilivyoingia mwili wake bado unaendelea kufanyika” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha Jeshi hilo limeahidi kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote atakaye bainika kupanga, kuratibu na kutekeleza uhalifu huo, awe ni mwanafamilia, kutoka ndani ya chama, nje ya chama, ndani ya nchi au nje ya nchi.

Hukumu vigogo Chadema: Jaji asogeza hadi saa saba, Mdee ameaga
Mgonjwa wa kwanza wa Corona afariki Afrika