Utawala wa kijeshi nchini Niger, mashirika ya kiraia na wananchi wamekusanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Niamey, ili kutetea uhuru wa Taifa lao na kukabiliana na uingiliaji wa kigeni katika masuala ya ndani.

Wito huo wa maandamano ya kuunga mkono mapinduzi tayari umeitikiwa na mamia ya watu katika mji mkuu wa Niger Niamey, huku baadhi yao wakibeba bendera za Urusi, kuadhimisha uhuru wa nchi hiyo wa mwaka 1960.

Wananchi wakishangilia sambamba na Wanajeshi wa Taifa la Mali. Picha ya Moussa Kalapo/Reuters.

Huku hayo yakiendelea, tayari Kiongozi wa kijeshi muongoza mapinduzi, Jenerali Abdourahmane Tchiani, amezikemea baadhi ya nchi jirani na jumuiya ya kimataifa na kutoa wito kwa raia wa Niger kuwa tayari kulilinda taifa.

Tchiani amesema Niger itakabiliwa na nyakati ngumu katika siku zijazo na kwamba misimamo ya uadui mkali ya wale wanaopinga utawala wake haina maana na kwamba vikwazo vilivyowekwa wiki iliyopita na Jumuiya ya Afrika Magharibi – ECOWAS, ni haramu na vya kinyama.

SKUDU: Tutaipasua Azam FC mapema tu
Christopher Nkunku azua hofu Chelsea