Jeshi la nchini Guatemala limesema litapiga marufuku shughuli za kutoa mimba zinazofanywa na kundi la madaktari wa kigeni na wauguzi wanaowasili nchini humo kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji mimba bure kwa wanawake wakiwa na mimba changa.

Shirika hilo lenye makao makuu yake nchini Uholanzi liitwalo Women on Waves, lilijitolea kuwachukua wanawake wajawazito kwa boti mpaka kwenye eneo la kimataifa la bahari, ambapo zoezi hilo hufanyika bila kuvunja sheria za nchi hiyo.

Aidha, kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, utoaji wa mimba huruhusiwa pale ambapo maisha ya mama yako hatarini

Wataalam hao wamesema vitendo vya utoaji mimba kiholela huhatarisha maisha ya zaidi ya wanawake 60,000 wa Guatemala kila mwaka

Marekani yasitisha zoezi la kuwarudisha makwao raia wa kigeni
Mrema amshukia tundu Lissu kuhusu watuhumiwa wa dawa za kulevya