Mshambuliaji kutoka England, Jesse Lingard, kesi yake imeanza kusikilizwa mahakamani baada ya kudaiwa kutoa jina la uwongo alipokamatwa na askari kutokana na kuendesha gari kwa spidi kali.

Lingard anayekipiga Nottingham Forest aliambiwa na mahakama atoe maelezo kutokana na kitendo chake cha kuendesha gari aina ya Range Rover kwa spidi.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester United na West Ham, anadaiwa kuwapa polisi jina la mtu ambaye hapatikani katika anwani ambayo pamoja inaaminika kuwa ni eneo la kuegesha magari.

Kesi yake ilisikilizwa kwa mara ya kwanza na Mahakama ya Stockport wikiendi iliyopita ingawa nyota huyo aliwakilish- wa na mwanasheria wake.

Mahakama ilipata taarifa kwamba gari aina ya Range Rover ilikamatwa na polisi baada ya kuonekana kwenye kamera zilipo barabarani huko Old Trafford tangu mwaka jana, lakini Lingard hakusimamishwa na polisi kwa mujibu wa ripoti.

Mike Arden, wa kituo cha polisi cha Greater Manchester, alisema: “Jeshi lilimwandikia Lingard katika anwani yake ya nyumbani” ikiambatana na notisi ya kufunguliwa mashitaka na wakamuomba atoe maelezo ni nani aliyekuwa akiendesha gari.

Arden akaendelea kusema notisi hiyo ilionyesha wazi kwamba mtu ambaye ilielekezwa kwake hakuwa mhusika ambaye aliendesha gari hilo.

Endapo Lingard atakutwa na hatia atapokwa pointi sita kwenye leseni yake ya gari na atatoa faini ya Pauni 1,000.

Kibadeni bado kinara Simba SC Vs Young Africans
Job afunguka kilichombakisha Young Africans