Mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Arsenal, Gabriel Jesus amepata majeraha ya mguu na sasa atakosa mwanzo wa msimu wa Ligi Kuu England.

Jesus hakucheza mechi ya juzi Jumatano (Agosti 02) ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi dhidi ya Monaco ambapo Arsenal waliibuka na ushindi wa penalti 6-5 baada ya sare ya bao 1-1 dakika 90 za mchezo huo.

Majeraha ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yanafanana na aliyopata msimu uliopita ambayo pia yatahitaji upasuaji.

 Kocha Inter Miami amuhurumia Messi

“Ni pigo kubwa kwa sababu alishaanza kurejea kwenye ubora wake,” alisema Arteta.

Akizungumza baada ya mchezo huo Uwanja wa Emirate, Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta alisema Jesus alikuwa anajisikia maumivu kwenye mguu wake kwa wiki chache zilizopita.

“Kwa bahati mbaya, alifanyiwa uchunguzi mdogo asubuhi hii. Alisema kuwa anahisi maumivu ya mguu na tulilazimika kumtibu. Sio majeraha makubwa lakini atakuwa nje ya uwanja kwa wiki chache,” alisema Arteta.

Majeraha ya Jesus yametokea siku nne kabla ya pambano la Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City na siku 10 kabla ya Ligi Kuu England kuanza ambapo watacheza na Nottingham Forest.

Eddie Nketiah sasa anatazamiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Arsenal wakati huu ambapo Jesus atakuwa nje na alikuwa nahodha wa Arsenal kwenye mchezo dhidi ya Monaco huku kiungo Declan Rice na Jurrien Timber wakianza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu hiyo.

Ahmed Ally: Hatutaacha kitu 2023/24
AS Vita yaichorea ramani Singida FG