Jamii imetakiwa kuwa tayari ili kujikinga na maafa wakati wowote ikiwemo mlipuko wa matukio yatokanayo na majanga kama magonjwa ya binadamu na Wanyama.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameyasema hayo Jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja.
Amesema, “Tanzania kama Nchi imepitia historia ya kukabiliwa na matukio ya maafa yatokanayo na majanga na milipuko ya magonjwa ya binadamu na Wanyama hivyo ipo haja ya kuwa na mipango ya kitaifa ya kubaini viashiria ili kuzuia maafa yanayoweza kutokea.”
Dkt. Yonaz ameongeza kuwa, ufuatiliaji wa matukio yanayoweza kuathiri afya ya binadamu, wanyama na mazingira, unatakiwa kufanyika kwa ufanisi kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja wa 2022 – 2023.