Kiungo Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Jibril Sillah, raia wa Gambia, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu atue nchini kwa kusema kilichomleta kwenye klabu hiyo ni mipango endelevu na miundombinu aliyoiona, hivyo anaamini ni sehemu sahihi kwake kuweza kuipa mafanikio na kutangaza jina lake ndani na nje ya mipaka ya bara la Afrika.

Kiungo huyo alitua nchini Jumapili (Julai 02) na kwa mara ya kwanza alishuhudia mechi ya Fainali ya vijana chini miaka 20 kati ya Mtibwa Sugar na Geita Gold kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es salaam.

“Nilikuwa nimepata ofa nyingi lakini nimeona mpango wa maendeleo ya klabu hii na mimi bado ni kijana, kwa mipango na miundombinu yake imenivutia mimi pamoja na kocha wangu, hivyo nikasema acha niende Azam naweza kuendelea zaidi pale na kuzidi kutangaza jina langu,” alifichua mchezaji huyo sababu za kukubali kujiunga na klabu hiyo.

“Nashukuru kila mmoja, mashabiki na watu wote waliofanikisha hili, nimekuja hapa kwa sababu namfahamu vizuri kuhusu klabu hii, kwa hiyo nimekuja kuisaidia timu ili tuandike historia kwa pamoja tushinde mataji pamoja na iendelee kukua,” amesema mchezaji huyo.

Mchezaji huyo anayekipiga pia kwenye wa klabu Timu ya Taifa ya Gambia chini ya miaka 23, alikuwa akiichezea Klabu ya Jeunesse Sportive ya Morocco kwa mkopo kutoka klabu Raja Athletic Club.

Ajali ya boti: Wahamiaji 73 hawajulikani walipo
Jorge Mas: Haikuwa rahisi kumsajili Messi