Serikali imepongeza juhudi zinazofanywa na uongozi wa jiji la Mwanza katika kuhakikisha linapunguza uharibifu na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na shughuli mbalimbali za kijamii.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika ujenzi wa dampo la machinjio ya kisasa jijini humo.

Amesema kuwa maandalizi ya ujenzi na miundombinu ya dampo la kisasa kama mizani ya kupimia taka, ofisi na maabara ya kemikali katika dampo hilo yako vizuri hivyo yamepelekea jiji hilo kufuzu kupata ufadhili kupitia Benki ya dunia licha ya kutumia mapato ya ndani.

“Naamini katika mradi huu unaokuja wa zaidi ya shilingi Bilioni 19.8 miundombinu ya hapa itakuwa ni mizuri na rafiki zaidi kwa mazingira, kikubwa zaidi ni kuwekeza nguvu zetu katika mradi huu na kuhakikisha kuwa unatekelezwa kama ulivyopangwa,”amesema Mpina

Aidha, Katika hatua nyingine Mpina pia amewapongeza wahisani kwa kuiamini Serikali ya awamu ya tano katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika suala zima la hifadhi ya mazingira.

Hata hivyo, amesesisitiza utunzaji wa mazingira uzingatiwe katika shughuli mbalimbali za uzalishaji hasa viwandani ili kuweza kuepuka madhara mbalimbali ya kiafya yanayoweza kujitokeza pindi tu mazingira yatakapoharibiwa.

 

Magazeti ya Tanzania leo Agosti 6, 2016
Julio apeta, wengine waenguliwa uchaguzi TFF