Meneja wa Man Utd Jose Mourinho, amemjumuisha kiungo kutoka nchini Ujerumani Bastian Schweinsteiger katika orodha ya wachezaji 25 wa klabu hiyo, ambao wanapaswa kucheza michezo ya ligi kuu ya soka nchini England (PL), msimu wa 2016/17.

Schweinsteiger alizusha zogo miongoni mwa wadau wa soka dhidi ya Mourinho, kufuatia kuenguliwa kwake katika michezo ya kabla ya baada ya kuanza kwa msimu huu.

Pamoja na kuibuka kwa mzozo huo, bado kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, aliendelea kuwa sehemu ya Man Utd na alipelekwa kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba.

Mchezaji mwingine aliyeorodheshwa na Mourinho katika kikosi cha Man Utd kitakachoshiriki ligi kuu ya England (PL) msimu huu ni Sadiq El-Fitouri, ambaye alisajiliwa akitokea Salford City, klabu ambayo inamilikiwa na magwiji wa Old Trafford Gary Neville, Phil Neville, Ryan Giggs, Nicky Butt pamoja na Paul Scholes.

Mourinho, Guardiola, Conte Waanza Kukabana England
Gianluigi Buffon: Ninatamani Kucheza Klabu Moja Na Balotelli