Lionel Messi anatarajia kushinda tuzo ya nane ya Ballon d’Or baadae mwezi huu baada ya majina ya washindi kwa upande wa wanaume na wanawake wa tuzo za mwaka huu wa 2023 kuvuja.

Messi mwenye umri wa miaka 36, ameonekana kushinda baada ya kuiwezesha Argentina kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia 2022 katika fainali zilizofanyika huko Qatar mwaka jana.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona na Paris Saint-Germain alijiunga na Inter Miami, Julai mwaka huu na tangu wakati huo amekuwa moto kwelikweli huko kwenye ligi ya MIS.

Baada ya kukosa tuzo ya mwaka 2022 iliyonyakuliwa na Karim Benzema, Messi anaripotiwa kwamba atanyakua tuzo hii ya mwaka huu, ambayo sherehe yake itafanyika jijini Paris, Ufaransa, Jumatatu ya Oktoba 30.

Messi akishinda basi atakuwa mchezaji wa kwanza kushinda Ballon dOr akiwa nịe ya Ulaya na hapo atakuwa ameweka pengo la tuzo tatu dhidi ya mpinzani wake Cristiano Ronaldo.

Na kwenye kinyang’anyiro cha mwaka huu, Messi anaripotiwa kumpiku straika wa Manchester City, Erling Haaland na mchezaji mwenzake wa zamani wa PSG, Kylian Mbappe.

Haaland alishinda mataji matatu akiwa na kikosi cha Man City mwaka jana baada ya kufunga mabao 52 katika mechi53.

Wakati Mbappe, alifunga hat-trick kwenye fainali ya Kombe la Dunia walipokabiliana na Argentina ya Messi na alifanya vizuri alipokuwa na kikosi cha PSG, lakini Messi amekuwa na nafasi kubwa ya kushinda baada ya kuipa Argentina ubingwa wa Kombe la Dunia na alifunga mabao muhimu katika fainali hizo.

Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 19, 2023
Jobe kumfuata kaka yake Real Madrid