Katika hali ya kawaida watu wengi wamezoea kusikia na kuambiwa kuwa Chocolate si kitu kizuri na kuna sababu nyingi za kukufanya uamini kuwa chocolate si nzuri.
Watu husema inaharibu meno, wengine hudai kuwa inasababisha kisukari na wengine huenda mbali zaidi wakidhani kuwa inaharibu ngozi kutokana na wingi wa mafuta iliyo nayo.
Ukweli ni kwamba Chocolate si mbaya kwa afya yako na hii inatokana na matokeo ya utafiti rasmi (research) ambayo yamekuja na faida hizi nne ambazo zitakufanya ule chocolate mara nyingi zaidi uwezavyo.
Hizi ni faida za Chocolate
Chocolate ni nzuri kwa Moyo wako
Utafiti unaonyesha kuwa chocolate inaweza kusaidia kupunguza magonjwa ya moyo na hata shinikizo la damu na shambulio la moyo (Heart Attack).
Chocolate nyeusi zimethibitika kuwa na uwezo wa kusaidia moyo ambao umeanza kuathirika na matatizo ambayo yanaweza kukuletea ugonjwa wa kiungo hicho muhimu kwenye mwili wa binadamu.
2.Inapunguza kisukari.
Ni vigumu kuamini lakini ukweli halisi ni kwamba , chocolate inasaidia kuondoa uwezekana wa mtu kupata kisukari.
Watu ambao wamekuwa na kawaida ya kula chocolate walau kipande kidogo mara moja kwa siku kwa muda wa siku tano wanakuwa na uwezo wa kuwa na kinga dhidi ya kisukari kuliko wale ambao hawali chocolate kabisa.
Kupambana dhidi ya Msongo wa mawazo (stress).
Tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa chocolate inasaidia kupunguza msongo wa mawazo au stress.
Watu wenye msongo wa mawazo hushauriwa kula walau gramu 45 za Chocolate kila siku wa muda wa wiki mbili ili kushusha msongo wa mawazo.
Imesemekana kuwa Watu wanaokula Chocolate mara kwa mara huwa wembamba, hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya.
Takribani watu 1000 nchini Marekani walifanyiwa utafiti ambao wamekuwa makini katika vyakula vyao. Waliokuwa wakila Chocolate mara kwa mara walipatikana wakiwa wembamba kuliko wenzao ambao hula Chocolate baada ya muda.
Wanasayansi wanasema, japo Chocolate ina sukari nyingi, ina viungo ambavyo husaidia kupunguza uzito wa mwili, lakini siyo kuchoma mafuta.
Flavonoids ambazo zinatumika kutengeneza chocolate zina chembechembe ya vimelea (microorganisms) vinavyoweza kusaidia ngozi na kuikinga dhidi ya miale ya jua