Wataalamu wa afya wanaeleza, kuwa na tatizo la kiafya haikufanyi wewe kuwa mtu anayeweza kupata maambukizi ya virusi vya Covid 19 kuliko mtu mwingine yeyote.

Lakini inaonekana wale ambao mfumo wao wa kinga ya mwili umedhoofika na watu wenye magonjwa ya kudumu ukiwemo moyo, kisukari, au pumu wana hatari zaidi ya kuathiriwa.

Wagonjwa wa pumu wanashauriwa kutumia inhaler ya kuzuia (ambayo kwa kawaida ina rangi nyekundu ) kila siku kama walivyoagizwa na daktari.

Hii itakusaidia kupunguza hatari ya shambulio la pumu linaloweza kusababishwa na virusi vya aina yoyote vinavyoweza kushambulia mfumo wa kupumua , vikiwemo coronavirus.

Inashauriwa kuwa wakati wa matembezi, tembea na inhaler yako ya rangi ya bluu kila wakati, ili utakaposikia dalili ya shambulio la pumu uitumie mara moja.

Lakini kama pumu yako itakuwa mbaya zaidi inaweza kua una coronavirus, na hivyo basi unatakiwa kupiga simu kwenye namba za huduma za tiba ya coronavirus katika nchi yako, kwa Tanzania ni 199 bure.

 

Papa aendesha Misa ya pasaka kwa Video
Corona Kenya: Wawili wafariki msongamano wa kupokea chakula cha msaada