Imezoeleka kuwa wanawake pekee ndiyo wameumbiwa kuingia period kila mwezi mara pale wanapovunja ungo, kudhihirisha kuwa sasa wako tayari kuweza kubeba ujauzito na kuzaa.
Nikujuze tu kuwa hata wanaume nao hupata mabadiliko katika via vyake vya uzazi (hedhi), lakini sio kama ile ya wanawake ambapo wao hutoka damu sehemu zake za siri (baada ya yai kutorutubishwa na kutoka).
Hii ni kwa mujibu mtaalamu wa psychotherapist na mwandishi wa kitabu cha Male Syndrome (IMS), Jed Diamond, PhD. Diamond, amedhirisha hili na kusema kwamba wanaume nao huingia period lakini ni tofauti na ile ya wanawake.
Kwa wanaume wao hukutana na mabadiliko ya homoni za testosterone ambazo husababisha mabadiliko ya kiafya, ikiwemo kuwa na msongo wa mawazo, uchovu na kubadilika kwa hali kila mara.
Hali hii pia huwatokea wanawake pale wanapoingia hedhi na muda mwingine huwaletea maumivu makali ya tumbo kutokana na mabadiliko ya mwili katika via vyake vya uzazi, lakini kwa wanaume haina madhara makubwa na wala hawawezi kupata damu kama wanawake, zaidi ya kuhisi mabadiliko kutokana na kutotulia kwa homoni.