Kabichi ni mboga ya majani na unaweza ukala pekeyake, asili ya mboga hii ni bara la Ulaya na inakadiriwa ilianza kutumiwa na binadamu tangu miaka ya 100 kabla ya kristo.
Kabichi hufanya kazi ya kupunguza kiasi cha sukari mwilini, huboresha afya ya moyo na macho, hutibu matatizo ya choo kigumu na husaidia kupona haraka kwa vidonda.
Vilevile husaidia kupunguza uzito wa mwili kwa watu walio na uzito uliozidi pamoja na kuharibu sumu zinazoua seli za mwili.
Inaweza kutumika kama tiba asili kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo, juisi yake pamoja na kuwa na aina nyingine za virutubisho muhimu pia ina viambata muhimu vinavyosaidia kuponya majeraha ya vidonda vya tumbo.
Juisi yake ambayo inatokana na maji yake yaliyochemshwa ina vitamini U ambayo inashauriwa kunywa mara mbili kwa siku.
Mboga hii pia ina vitamini K ambayo inasaidia damu kuganda endapo mtu akapata jeraha.
Imeelezwa kuwa kipande kidogo tu cha kabichi kinatosha kuongeza zaidi ya microgram 38.2 za vitamini K, hivyo basi kwa mtu ambaye damu yake akipata jeraha haigandi kwa wastani wa muda wa dakika tatu anashauriwa kuanza kula kabeji.
Hali kadhalika majani ya kabichi huwa na kemikali zinazoitwa glucosinolate ambazo huondoa uvimbe na maumivu ya matiti ambayo huwapata hasa wanawake wanao nyonyesha, waliomaliza na wasichana wadogo ambao kwa mara kadhaa huvimba.
Inashauriwa kuyaweka majani ya kabichi kwenye moto, yakichemka jikande kwa dakika 5 mara mbili kwa siku hadi pale tatizo litakapo malizika.