Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeweka mkazo wa kumtoza faini ya shilingi 50,000 mtu yoyote atakayekamatwa akitupa taka hovyo.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Isaya Mngurumi jana alisisitiza kuwa watamchukulia hatua mtu anayechafua manisapaa hiyo kwa kutupa taka hovyo huku akiahidi zawadi ya shilingi 25,000 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu anayetupa taka hovyo.

Mngurumi aliongeza kuwa wameweka mpango wa kudhibiti utupaji taka kwenye mabasi na vituo vya daladala kwa kuweka vifaa vya kutupia taka ndani ya daladala na mabasi hayo. Alisema kuwa abiria wote watakaotupa taka hovyo ndani ya daladala watatozwa faini.

“Kutakuwa na vituo vitatu vya ukaguzi ndani ya magari ili kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa, vituo hivyo ni Kariakoo, Mnazi Mmoja na Posta,” alisema Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Rais Asitisha Mchezo Wa Soka Dakika Ya 63
Mwanzilishi wa Facebook Atangaza Kuwapa Masikini 99% ya hisa zake