Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Jakaya Kikwete amekubali shamba lake la mifugo lililopo kijijini kwake Msoga Bagamoyo litumike kama shamba darasa.

Kikwete amekubali ombi la shamba hilo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo mkoani Morogoro baada ya kutembelea chuoni hapo akiwa na wataalamu wake wa mifugo kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kuhusu kilimo na mifugo.

Aidha,Uongozi wa SUA umetumia nafasi hiyo kuwasilisha ombi lao kwa Rais mstaafu Kikwete ambaye alikubali na kuingia makubaliano ya pamoja ili kulitumia shamba lake la mifugo kama shamba darasa la kutolea elimu ya vitendo kwa wanafunzi na wataalamu wa mifugo

Hata hivyo, Rais Mstaafu Kikwete kwa sasa amejikita zaidi kwenye suala la ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa, kilimo cha mazao ya chakula na matunda hasa mananasi kijijini kwake Msoga, Chalinze , wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 23, 2017
Kafulila aitosa Chadema