Tasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete – JKCI, inatarajia kuanza kutoa huduma ya kuzibua mishipa ya uume kama njia mojawapo wa kukabiliana na upungufu wa tatizo hilo kwa wanaume.

Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge, ameyasema hayo hii leo jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa huduma hiyo inatarajiwa kuanza Oktoba 2023.

Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Peter Kisenge.

Amesema, “tutaanzisha huduma kwa kushirikiana na wenzetu wa India, tatizo la nguvu za kiume linazidi kuongezeka kwa mishipa ya uume kuziba lipo pengine ni siri ya wagonjwa hatuwezi kuweka wazi ila huduma itaanza mwaka huu.”

Aidha Dkt. Kisenge amesema, tatizo la Wanaume kukosa nguvu za kiume ni kubwa japo hakuna utafiti walioufanya, lakini wapo wanaofika JKCI kuulizia huduma hiyo.

Wawili wapoteza maisha ajali ya Basi na Lori Kibaha
Mhagama awapongeza Watoto kampeni GGML KiliChallenge- 2023