Uongozi wa timu ya JKT Tanzania, umeweka wazi malengo yao ya kuwa mabingwa wa Ligi ya Championship msimu huu yametimia kwa asilimia 90.

Katibu wa JKT Tanzania, Kapteni Speratus Lubinga, amesema kikosi kimejipanga kufanya vema kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika michezo mitatu iliyobaki.

“Sina mengi lakini natoa shukrani za dhati kwa uongozi mzima wa Jeshi la Kujenga Taifa likiwa chini ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele pamoja na Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambao wamekuwa wakituongoza”

“Kikosi kipo imara, lengo ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi na kuwa mabingwa wa Ligi ya Championship msimu huu kwani tutakuwa tumetimiza maagizo ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ambaye alitaka kuona kikosi kinarejea ligi kuu msimu ujao, sina mashaka na wachezaji kwani wanajituma kuhakikisha timu inarudi ligi kuu,” amesema

JKT TZ ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa wana alama 61, na sasa wanahitaji alama moja tu kujihakikishia kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara Bara msimu ujao 2023/24.

Nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi ya Championship ipo Pamba FC yenye alama 51, huku kila timu ikibakiza michezo ya tatu kumalizika kwa ligi.

Serikali kusapoti Riadha U-18 na U-20
Majaliwa ataka weledi, Ubunifu matokeo chanya kimaendeleo