Klabu ya JKT Tanzania imetamba kuiduwaza Simba SC katika mchezo wa kufunga Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kesho Jumanne (Mei 28), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mchezo huo utakaoanza kurindima saa kumi jioni, utakuwa na malengo makuu mawili tofauti, ambapo kwa upande wa Simba SC watahitaji kushinda ili kuendelea kuifukuzia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, zote zikiwa na alama 66 kila mmoja.

Upande wa JKT Tanzania wenye alama 32 watahitaji kuibuka na ushindi ili kujiondoa katika eneo la hatari kwenye msimamo wa Ligi hiyo, kwa kuepuka kucheza Play Off, wakiiacha Kagera Sugar kwa tofauti ya alama moja.

Malengo hayo mawili tofauti yananogesha ushindani katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka Tanzania Bara, huku JKT Tanzania wakitumia Kurasa zao za Mitandao ya Kijamii kutamba kushinda na kuiduwaza Simba SC.

Kupitia Ukurasa wao wa Instagram JKT wameandika wapo tayari kwenda kuwafurahisha Mashabiki zao.

“Mchezo muhimu sana kwetu dhidi ya Simba tunaenda kufunga msimu kwa surprise kubwa kwa mashabiki wetu.

Tuwaambie tu hii mechi KUNA MKUBWA ATANG’ANG’ANIWA 💪

Kocha Simba SC atangaza vita na wanajeshi
Mzize awajibu mashabiki wanaombeza