Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza kusitisha kwa muda mafunzo ya jeshi hilo ya kujitolea kwa mwaka 2020/2021 mpaka hapo itakapotangaza tena.

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 19, 2021 jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena, wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisi za makao makuu ya jeshi hilo.

Kanali Mabena ameeleza kuwa mafunzo hayo yamesitishwa kutokana na sababu za ndani.

Kutokana na kusitishwa kwa safunzo hayo JKT imewataka vijana walioripoti makambini kurejea majumbani na wale ambao hawajaripoti wasiende kuripoti.

Danny Drinkwater atimkia Uturuki
Mfahamu Sebastien Desabre anaewanyima usingizi Simba SC