RAIS wa Barcelona, Joan Laporta ameshtakiwa kwa tuhuma za kuwahonga waamuzi kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.
Taarifa za mshtuko zimeibuka asubuhi ya jana kupitia Shirika la Utangazaji (EFE) la Hispania kwamnba hakimu katika kesi hiyo anayefahamika kwa jina la Caso Negreire ameamua kumfungulia mashtaka bosi huyo mwenye umri wa miaka 61.
Imebainika bosi huyo anatuhumiwa kwa rushwa, ufisadi katika michezo, utawala usio wa haki na kughushi hati za kibiashara.
Laporta aliyeingia kwenye awamu ya pili ya Urais Barcelona mwaka 2021 alikuwa madarakani mwaka 2003 hadi 2010.
Kesi ya Caso Negreira inahusisha malipo wenye ya takriban Pauni 63 milioni kwa makamu wa rais wa zamani wa kamati ya ufundi ya waamuzi Jose Maria Enriquez Negreira na mtoto mwanawe. Malipo hayo ambayo yalikuwa katika kipindi cha miaka 18 yalichunguzwa ili kubaini ukweli wa mambo unaomhusu Laporta.
Hiyo imekuja baada ya Barcelona kushtakiwa kwa kuendeleza ufisadi kwenye soka Aprili mwaka huu wakati UEFA ilipoanza uchunguzi.
Licha ya kashfa hiyo Bodi ya UEFA iliiruhusu Barca kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
Jaji Joaquin Aguirre, alipendekeza shtaka la kuendeleza ufisadi kwenye michezo ibadilishwe na kuwa hongo.