Klabu ya Real Madrid imeripotiwa kuvutiwa kumsajili mdogo wake Jude Bellingham ambaye ni Jobe Bellingham.

Scaut ya Madrid imekuwa ikimfuatilia kiungo huyu anayekipiga katika klabu ya Sunderland FC kwenye mechi za timu ya Taifa ya Uingereza UI9.

Jobe ameekuwa na mwenendo mzuri akiwa na Sunderland inayoshiriki Championship msimu huu ambao ni wa kwanza kwake. Kama ambavyo imekuwa kwa Jude pale Real Madrid.

Skauti wa Madrid, Juni Cafalat amesema kwa jicho lake baada ya kumtazama dogo huyo akiwa Sunderland na timu ya taifa amekiri kuwa baada ya muda atakuwa na staa mkubwa duniani.

Kama mambo yatakwenda sawa, pengine dirisha dogo tukashuhudia Bellingham wawili wakicheza Santiago Bernabeu na kuwa rekodi kwa klabu hiyo kuwa na ndugu wawili kwenye klabu moja.

Jina la Messi limevuja Ballon d'Or
Jesse Lingard kutimkia Saudi Arabia