Mchezaji wa timu ya Maaya Wanawake ya England, Jodie Taylor ametangaza kustaafu rasmi mchezo wa soka.

Taylor amepita timu tofauti katika nchi sita na amemalizia soka lake katika klabu ya Arsenal alipocheza mara ya mwisho msimu uliopita.

Mshambuliaji huyo amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 37 baada ya kucheza mechi 51 katika kikosi cha England ikiwemo kubeba tuzo ya kiatu cha dhahabu mwaka 2017 katika michuano ya Euro.

Alisema amefikia hatua ya kutangaza kustaafu mchezo wa soka na kuwaachia wengine waendelee pale alipoishia na kufikia malengo waliyojiwekea.

“Ninafurahia Kutangaza rasmi kustaafu mchezo wa soka japokuwa niliupenda kwa muda wote.

“Ninafikiri kitu kizuri zaidi ni kustaafu kwa furaha na kuwaachia wengine waweze kuendeleza pale nilipoachia mimi na kufikia malengo waliyojiwekea,” amesema.

Mchezaji huyo aliyewahi kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa Wanawake akiwa na Lyon, alianza kucheza soka akiwa na umri wa miaka 15 katika kikosi cha Tranmere Rovers kabla ya kutimkia Marekani alipokwenda kwa ufadhili wa masomo.

Gamondi ashindilia msumari Ligi ya Mabingwa
Simba, Young Africans zimeleta AFCON 2027