Rais wa Marekani Joe Biden ametetea uamuzi wake uliokosolewa kwa kiasi kikubwa wa kuwatoa wanajeshi wa Marekani kutoka Afghanistan tukio ambalo lilisababisha kuanguka ghafla kwa serikali ya nchi hiyo.
Tangu Agosti 15, wakati mji mkuu Kabul, ulipoanguka hatua zilianza kuchukuliwa na jeshi la Marekani ili kuwaondoa zaidi ya watu 120,000 raia wa Marekani na Waafghanisatan ambao walikuwa wakifanya kazi kwao.
Biden amesema alikubali uamuzi huo kwa sababu kukaa muda mrefu nchini Afghanistan haikuwa nia yao, ingawa vikosi vya usalama vya Afghanistan vilianguka haraka kuliko ilivyotarajiwa, Marekani ilikuwa tayari kwa hali hiyo.
Biden aliahidi kuwahamisha Wamarekani walioachwa nchini Afghanistan na kwa Waafghanistan wenyeji ambao wanataka kuondoka.
Wakati kukiwa na ukosoaji kwamba uokoaji unapaswa kuanza mapema, Biden amesema bado kungekuwa na hali ya kukimbilia uwanja wa ndege. Pia kulikuwa na vitisho kwa Marekani kutoka kwa wanamgambo wa Kiisilamu, Biden amesema mkakati wa Marekani ilibidi ubadilike hakukuwa na haja ya kuwa na wanajeshi kwaajili ya kupambana na ugaidi
Na akizungumzia washirika wa IS ambao walishambulia umati katika uwanja wa ndege wa Kabul na kuua zaidi ya watu 170, 13 kati yao wanajeshi wa Marekani Biden amesema bado hawajamalizana nao.