Rapa Joe Budden amemvaa tena Eminem kupitia kipindi chake anachokiweka mtandaoni cha ‘Joe Budden Podcast’, akidai kuwa sio saizi yake na kumtishia kipigo.

Budden ameendelea kujibu mapigo baada ya Eminem kumchana kwenye wimbo wake wa ‘Fall’ aliomtaja jina kabla ya kumpa za uso. Rapa huyo amedai kuwa yeye amekuwa rapa bora zaidi ya Eminem kwa miaka zaidi ya kumi sasa.

“Taarifa kwa Em. Nimeisikiliza albam, na kwasababu ninadhani hauwafahamu wanafamilia wote wa kundi [la D12], sidhani kama unaifahamu historia,” alisema Budden.

“Ngoja nikwambie ambacho Joe Budden anafakiria muda wote. Nimekuwa rapa bora zaidi yako kwa wakati wote katika kipindi cha muongo mzima,” aliongeza.

Budden hakuishia hapo, aliendelea kutoa maneno machafu dhidi ya Eminem akimtaka kutojaribu kumjibu tena kupitia nyimbo zake badala yake ajibu kwa njia nyingine kwani akifanya hivyo tena; kwa kuhuisha msemo huo na msemo maarufu hapa kwetu ni ‘atapata kipigo cha mbwa koko’.

“Kwa kipindi kingine ukitaka kunizungumzia, ufanye nje ya albam yako. Ukifanya tena mara ya pili, nitakudandia wewe. Nitakupa kipigo kikali,” alifunguka kwa maneno yenye ukakasi ambayo tumeyaondoa kwenye tafsiri hii.

Alimtaka Eminem kuendelea kufanya jitihada kwenye nyimbo zake akimkejeli kuwa, “wakati mwingine utakapoghani hakikisha unatoa kitu ambacho kinaniamsha gwiji mimi kitandani.”

Mgogoro kati ya wakali hao ulishika moto baada ya Budden kuikosoa vikali albam ya Eminem ‘Revival’ akidai kuwa ni takataka.

Ikumbukwe kuwa Eminem aliwahi kuwa Bosi wa Budden aliyekuwa na kundi lake la SlaughterHouse.

Video: DC Katambi amsweka ndani aliyetaka kuvuruga mkutano wake na wananchi
Video: JPM aweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Barabara mkoani Mara