Mlinda mlango kutoka nchini England Joe Hart ameikataa klabu ya Sunderland ambayo ilikua tayari kumbakisha nyumbani, na badala yake alichagua kujiunga na Torino ya Italia akitokea Man City .

Taarifa zilizochapishwa katika tovuti ya Skysports na kuripotiwa katika kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England mchana huu, zimeeleza kuwa meneja wa Sunderland David Moyes alikua tayari kumsajili Hart.

Sunderland walijipanga kumsajili mlinda mlango huyo kwa mkopo, kufuatia changamoto inayowakabili ya kuumia wa kipa wao chaguo la kwanza Vito Mannone ambaye anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

Hata hivyo klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko Stadium of Lights ilikua tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa kama sehemu ya kuchangia mshahara wa Harts ambao unapaswa kulipwa kila juma kwa kushirikiana na Man City, lakini bado mlinda mlango huyo alikataa ofa hiyo.

Hart mwenye umri wa miaka 29 hii leo anatarajiwa kusafiri hadi nchini Italia katika mji wa Turin kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya, kabla ya kukamilisha tarartibu za kusajiliwa kwa mkopo kwenye klabu ya Torino inayoshiriki ligi ya Sirie A.

Simba SC Yaitikia Agizo La Rais Magufuli Kwa Vitendo
Majaliwa apokea Sh. Mil. 50 kutoka NNSF