Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Joeboy amezungumza kufuatia onyesho lake katika tamasha la Nairobi ‘Afro Jam’ kukosa mvuto wa kutosha kutokana na kusikika vibaya kwa mfumo wa sauti (Sound System).

Akiwashukuru mashabiki wake wa Kenya kwa kujitokeza na kuleta muamko na shangwe kwenye hafla hiyo, nyota  huyo mmliki wa rekodi Sip (Alcohol), amewalaani baadhi ya waandaji kutokana na hitilafu ya mfumo wa sauti iliyojitokeza wakati akitumbuiza jukwaani.

Joeboy alibainisha kuwa sauti haikuwa nzuri na pia miongoni mwa wapiga vyombo (mpiga gitaa) alikuwa amelewa jambo lililosababisha kupiga chombo chake nje ya mpangilio sahihi.

Kupitia ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram , Joeboy alichapisha taarifa hiyo akisema, “Asante Kenya! Sauti ilikuwa mbaya lakini nguvu zenu zikuwa juu kama kawaida.” Na kuongeaza kwa kusema “Na kwa mpiga gitaa mlevi, (akitoa tusi) kwa kucheza takataka.”

Joeboy aliongoza tukio hilo pamoja na mrembo wa Kenya Nikita Kering, kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa The Hub.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba Disemba 13, 2021
Mtanzania ashinda mashindano ya ubunifu nchini Finland