Huwa inawagharimu wasanii wengi katika suala la kufanya kolabo katika nyimbo wanazoandaa na hii mara nyingi inaweza kutokea kuwa msanii mmoja kuwa busy na kazi zingine kipindi cha uandaaji wa kazi.

Wimbo Mpya wa Joh Makini Perfect Combo ni wimbo ambao ulirekodiwa kwa muda wa masaa manne  tu ambapo bidada Chidnma alimezeshwa maneno ya kiswahili na akaweza kuimba kiswahili kilichonyooka kwa muda usiozidi dk 20 kwa mujibu wa msanii Joh.

joh

Katika mahojiano aliyofanya na Ayo Tv Msanii huyo kutoka Arusha amesema uamuzi wa kuita Perfect Combo  ngoma hiyo inayosumbua maskio ya mashabiki wa Hip hop ni kutokana na ushirikiano mkubwa kati yake na Chidnma.

”Kila tulichokuwa tunafanya kilikua kinaenda smooth, yaani kombinesheni iliyokamilika, ndio maana ikawa Perfect Combo” alisema Joh Makin

Joh Makin pia amesema kuwa wimbo huo aliandika miaka wimiwi iliyopita wakati alipokutana na mwanadada Chidnma Coke studio na ikawa rahisi kuweza kufanya naye wimbo huo kutokana kwamba pia walikuwa wakishirikiana kwa ukaribu zaidi.

Exclusive: Stand Utd Kampuni Waishangaa TFF
Luis Enrique: Ni Wakati Sahihi Kwa Messi Kustaafu