Mwamba wa Kaskazini, Joh Makini amefunguka kuhusu moja ya mijadala iliyopata nafasi zaidi kwenye vyombo vya habari kwa miaka mingi kuhusu kinachoweza kutokea kati yake na Tajiri wa Mashairi, Fid Q.

Joh amefunguka kupitia The Playlist ya 100.5 Times Fm kuwa kwanza hakuna na hakujawahi kuwepo mgogoro wowote kati yake na Fid Q na kwamba kutokuwepo kwa kolabo kati yao kumetokana na uhalisia wa mazingira yao kwa wakati husika.

“Mimi kama msanii na yeye kama msanii anything can happen… chochote kinaweza kutokea anytime (muda wowote). Ni vile tu hatujawahi kukutana kwenye hiyo vibe,” Joh alifunguka.

“Hatujawahi kuwa labda kwenye hiyo chemistry ya kusema tufanye ngoma pamoja, kwa hiyo huwezi jua,” aliongeza ambaye sasa wimbo wake wa ‘Mipaka’ umetuliza mitaa gambani.

Mwaka jana, Fid Q alifanya mahojiano na The Playlist na akaeleza kuwa hana tatizo na Joh Makini na kwamba yeye ndiye alikuwa chanzo cha Joh kuingia Coke Studio Africa baada ya kumpendekeza kwa waandaji.

Alieleza kuwa alitakiwa ajiunge na Coke Studio lakini alikuwa nje ya nchi na asingeweza kurudi kwa muda, hivyo alipoambiwa apendekeze rapa atakayefaa yeye alimuona Mwamba wa Kaskazini kuwa hataiangusha Tanzania.

Ushiriki wa Coke Studio ulisababisha Joh afanye ‘Perfect Combo’ na Chidnma wa Nigeria.

CCM yaibuka kidedea uchaguzi mdogo
JPM: Sina mpango wa kuongeza muda wa kuwa madarakani