Mlinda Lango mpya wa Tabora United John Noble ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Enyimba amesema amefurahi kutua Tanzania, huku timu hiyo ikitamba kusajili 12 wapya wa kigeni.

Mlinda mlango huyo mahiri amepewa mwaka mmoja na timu hiyo ambayo imepanda daraja na kutinga Ligi Kuu kwa mara ya kwanza.

Meneja wa Tabora United, Rashid Hassan amesema wamemsajili mchezaji huyo kutokana na umahiri wake langoni na ndiye atakuwa chaguo la kwanza langoni.

“Tumedhamiria kusajili wachezaji mahiri katika timu yetu na huu ni mwanzo wa kutambulisha wachezaji wetu tunaowasajili,” amesema.

Rashid ameeleza kuwa wanataka kusajili wachezaji wa kigeni 12 ambao wataungana na wazawa na kuwa kikosi kizima wanataka kisizidi wachezaji 27 na kwamba muda muafaka ukifika watawatambulisha.

Mlinda mlango huyo ameeleza furaha yake kujiunga na Tabora United ambayo imepanda daraja na kushiriki ligi kuu msimu huu akisema atashirikiana na wenzake kuhakikisha timu haishuki daraja bali inafanya vizuri.

“Kwa nafasi yangu ya kuzuia mabao nalazimika kuhakikisha washambuliaji wa timu pinzani hawafanikiwi kufunga hakika ni jambo zuri sana kutua kwenye timu hii na nitahakikisha naonyesha kiwango changu cha juu sana uwanjani,”amesema

Sera unyoneshaji Watoto mahala pa kazi yaleta mafanikio
Serikali yataka maoni marekebisho Sheria ya Madini