Nahodha na kiungo wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) John Obi amekanusha taarifa za kuchangia kiasi cha dola za kimarekani 30,000, kwa ajili ya kusaidia maandalizi ya timu hiyo, ambayo itashiriki michuano ya Olimpiki itakayoanza juma lijalo nchini Brazil.

Obi ambaye ni sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria ambayo itashiriki mchuano hiyo, amesema hakuna ukweli wa suala hilo ambalo limeripotiwa na vyombo kadhaa vya habari duniani.

Amesema hajachangia kiasi chochote cha pesa na taarifa hizo alizipata kutoka kwa rafiki zake wa Nigeria ambao walijaribu kumpigia simu kwa ajili ya kujua kama ni kweli amekubali kuchangia fedha za maandalizi ya timu.

“Kwa mara ya kwanza nilizisikia taarifa hizi baada ya kupigiwa simu na watu wangu wa Nigeria,” Alisema Mikel alipokua kwenye kambi ya timu ya taifa iliopo nchini Marekani.

“Kwanza nilifikiria utani lakini msisitizo wa maswali kutoka kwao, ndio ulijulisha kuwepo kwa taarifa hizi ambazo kwangu zilinishangaza.

“Mpaka sasa sijafahamu nani alizizusha taarifa hizi, na sijui alikua na lengo gani kwangu. ”

Timu ya taifa ya Nigeria inatarajia kupambana na Japan, Sweden na Colombia katika hatua ya makundi ya michuano ya Olimpiki.

Video: Ole Sendeka atoa ushauri Chadema
Gonzalo Higuain Afichua Siri Ya Kuondoka SSC Napoli